وَٱلْعَٰدِيَٰتِ ضَبْحًۭا ﴿١﴾
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
Sura ya 100 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلْعَٰدِيَٰتِ ضَبْحًۭا ﴿١﴾
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
فَٱلْمُورِيَٰتِ قَدْحًۭا ﴿٢﴾
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
فَٱلْمُغِيرَٰتِ صُبْحًۭا ﴿٣﴾
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
فَأَثَرْنَ بِهِۦ نَقْعًۭا ﴿٤﴾
Huku wakitimua vumbi,
فَوَسَطْنَ بِهِۦ جَمْعًا ﴿٥﴾
Na wakijitoma kati ya kundi,
إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٌۭ ﴿٦﴾
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌۭ ﴿٧﴾
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ﴿٨﴾
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ ﴿٩﴾
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ ﴿١٠﴾
Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍۢ لَّخَبِيرٌۢ ﴿١١﴾
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Al-'Adiyat (العاديات) ni sura ya 100 ya Qur'ani. Ina aya 11 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, العاديات, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Al-'Adiyat ina aya 11.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Al-'Adiyat iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.