ٱلْقَارِعَةُ ﴿١﴾
Inayo gonga!
Sura ya 101 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلْقَارِعَةُ ﴿١﴾
Inayo gonga!
مَا ٱلْقَارِعَةُ ﴿٢﴾
Nini Inayo gonga?
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْقَارِعَةُ ﴿٣﴾
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
يَوْمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلْفَرَاشِ ٱلْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ ٱلْمَنفُوشِ ﴿٥﴾
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ ﴿٦﴾
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
فَهُوَ فِى عِيشَةٍۢ رَّاضِيَةٍۢ ﴿٧﴾
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ ﴿٨﴾
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌۭ ﴿٩﴾
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
نَارٌ حَامِيَةٌۢ ﴿١١﴾
Ni Moto mkali!
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Al-Qari'ah (القارعة) ni sura ya 101 ya Qur'ani. Ina aya 11 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, القارعة, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Al-Qari'ah ina aya 11.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Al-Qari'ah iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.