Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 91 ya Qur'ani

Sura Ash-Shams

Makkiyya Aya 15 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا ﴿١﴾

Naapa kwa jua na mwangaza wake!

وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا ﴿٢﴾

Na kwa mwezi unapo lifuatia!

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا ﴿٣﴾

Na kwa mchana unapo lidhihirisha!

وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا ﴿٤﴾

Na kwa usiku unapo lifunika!

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا ﴿٥﴾

Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!

وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا ﴿٦﴾

Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!

وَنَفْسٍۢ وَمَا سَوَّىٰهَا ﴿٧﴾

Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا ﴿٨﴾

Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا ﴿٩﴾

Hakika amefanikiwa aliye itakasa,

وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا ﴿١٠﴾

Na hakika amekhasiri aliye iviza.

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ ﴿١١﴾

Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا ﴿١٢﴾

Alipo simama mwovu wao mkubwa,

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَٰهَا ﴿١٣﴾

Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا ﴿١٤﴾

Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.

وَلَا يَخَافُ عُقْبَٰهَا ﴿١٥﴾

Wala Yeye haogopi matokeo yake.

Ash-Shams Aya 1 kati ya 15

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Ash-Shams

Sura Ash-Shams (الشمس) ni sura ya 91 ya Qur'ani. Ina aya 15 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, الشمس, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Ash-Shams

Sura Ash-Shams ina aya ngapi?

Sura Ash-Shams ina aya 15.

Je, Sura Ash-Shams ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Ash-Shams iko katika Juzuu ipi?

Sura Ash-Shams iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Ash-Shams wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp