Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 90 ya Qur'ani

Sura Al-Balad

Makkiyya Aya 20 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

لَآ أُقْسِمُ بِهَٰذَا ٱلْبَلَدِ ﴿١﴾

Naapa kwa Mji huu!

وَأَنتَ حِلٌّۢ بِهَٰذَا ٱلْبَلَدِ ﴿٢﴾

Nawe unaukaa Mji huu.

وَوَالِدٍۢ وَمَا وَلَدَ ﴿٣﴾

Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.

لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَٰنَ فِى كَبَدٍ ﴿٤﴾

Hakika tumemuumba mtu katika taabu.

أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌۭ ﴿٥﴾

Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?

يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًۭا لُّبَدًا ﴿٦﴾

Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.

أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ ﴿٧﴾

Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?

أَلَمْ نَجْعَل لَّهُۥ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾

Kwani hatukumpa macho mawili?

وَلِسَانًۭا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾

Na ulimi, na midomo miwili?

وَهَدَيْنَٰهُ ٱلنَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾

Na tukambainishia zote njia mbili?

فَلَا ٱقْتَحَمَ ٱلْعَقَبَةَ ﴿١١﴾

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?

فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾

Kumkomboa mtumwa;

أَوْ إِطْعَٰمٌۭ فِى يَوْمٍۢ ذِى مَسْغَبَةٍۢ ﴿١٤﴾

Au kumlisha siku ya njaa

يَتِيمًۭا ذَا مَقْرَبَةٍ ﴿١٥﴾

Yatima aliye jamaa,

أَوْ مِسْكِينًۭا ذَا مَتْرَبَةٍۢ ﴿١٦﴾

Au masikini aliye vumbini.

ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾

Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.

أُو۟لَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾

Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا هُمْ أَصْحَٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ ﴿١٩﴾

Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.

عَلَيْهِمْ نَارٌۭ مُّؤْصَدَةٌۢ ﴿٢٠﴾

Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.

Al-Balad Aya 1 kati ya 20

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-Balad

Sura Al-Balad (البلد) ni sura ya 90 ya Qur'ani. Ina aya 20 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, البلد, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-Balad

Sura Al-Balad ina aya ngapi?

Sura Al-Balad ina aya 20.

Je, Sura Al-Balad ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-Balad iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-Balad iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-Balad wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp