Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 89 ya Qur'ani

Sura Al-Fajr

Makkiyya Aya 30 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلْفَجْرِ ﴿١﴾

Naapa kwa alfajiri,

وَلَيَالٍ عَشْرٍۢ ﴿٢﴾

Na kwa masiku kumi,

وَٱلشَّفْعِ وَٱلْوَتْرِ ﴿٣﴾

Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja,

وَٱلَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾

Na kwa usiku unapo pita,

هَلْ فِى ذَٰلِكَ قَسَمٌۭ لِّذِى حِجْرٍ ﴿٥﴾

Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?

إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ ﴿٧﴾

Wa Iram, wenye majumba marefu?

ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَٰدِ ﴿٨﴾

Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?

وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ ﴿٩﴾

Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?

وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾

Na Firauni mwenye vigingi?

ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَٰدِ ﴿١١﴾

Ambao walifanya jeuri katika nchi?

فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ ﴿١٢﴾

Wakakithirisha humo ufisadi?

فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾

Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.

إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾

Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.

فَأَمَّا ٱلْإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾

Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!

وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَٰنَنِ ﴿١٦﴾

Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!

كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ ﴿١٧﴾

Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,

وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾

Wala hamhimizani kulisha masikini;

وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًۭا لَّمًّۭا ﴿١٩﴾

Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,

وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّۭا جَمًّۭا ﴿٢٠﴾

Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.

كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّۭا دَكًّۭا ﴿٢١﴾

Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,

وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّۭا صَفًّۭا ﴿٢٢﴾

Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,

وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍۢ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾

Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?

يَقُولُ يَٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى ﴿٢٤﴾

Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!

فَيَوْمَئِذٍۢ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌۭ ﴿٢٥﴾

Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌۭ ﴿٢٦﴾

Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.

يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفْسُ ٱلْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾

Ewe nafsi iliyo tua!

ٱرْجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةًۭ مَّرْضِيَّةًۭ ﴿٢٨﴾

Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.

فَٱدْخُلِى فِى عِبَٰدِى ﴿٢٩﴾

Basi ingia miongoni mwa waja wangu,

وَٱدْخُلِى جَنَّتِى ﴿٣٠﴾

Na ingia katika Pepo yangu.

Al-Fajr Aya 1 kati ya 30

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-Fajr

Sura Al-Fajr (الفجر) ni sura ya 89 ya Qur'ani. Ina aya 30 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, الفجر, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-Fajr

Sura Al-Fajr ina aya ngapi?

Sura Al-Fajr ina aya 30.

Je, Sura Al-Fajr ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-Fajr iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-Fajr iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-Fajr wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp