Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 88 ya Qur'ani

Sura Al-Ghashiyah

Makkiyya Aya 26 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْغَٰشِيَةِ ﴿١﴾

Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?

وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ ﴿٢﴾

Siku hiyo nyuso zitainama,

عَامِلَةٌۭ نَّاصِبَةٌۭ ﴿٣﴾

Zikifanya kazi, nazo taabani.

تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةًۭ ﴿٤﴾

Ziingie katika Moto unao waka -

تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ ءَانِيَةٍۢ ﴿٥﴾

Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍۢ ﴿٦﴾

Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.

لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِى مِن جُوعٍۢ ﴿٧﴾

Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.

وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۢ نَّاعِمَةٌۭ ﴿٨﴾

Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.

لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌۭ ﴿٩﴾

Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,

فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍۢ ﴿١٠﴾

Katika Bustani ya juu.

لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةًۭ ﴿١١﴾

Hawatasikia humo upuuzi.

فِيهَا عَيْنٌۭ جَارِيَةٌۭ ﴿١٢﴾

Humo imo chemchem inayo miminika.

فِيهَا سُرُرٌۭ مَّرْفُوعَةٌۭ ﴿١٣﴾

Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,

وَأَكْوَابٌۭ مَّوْضُوعَةٌۭ ﴿١٤﴾

Na bilauri zilizo pangwa,

وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌۭ ﴿١٥﴾

Na matakia safu safu,

وَزَرَابِىُّ مَبْثُوثَةٌ ﴿١٦﴾

Na mazulia yaliyo tandikwa.

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾

Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?

وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾

Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?

وَإِلَى ٱلْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾

Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?

وَإِلَى ٱلْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾

Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?

فَذَكِّرْ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌۭ ﴿٢١﴾

Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾

Wewe si mwenye kuwatawalia.

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ﴿٢٣﴾

Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,

فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَكْبَرَ ﴿٢٤﴾

Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!

إِنَّ إِلَيْنَآ إِيَابَهُمْ ﴿٢٥﴾

Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ﴿٢٦﴾

Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!

Al-Ghashiyah Aya 1 kati ya 26

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-Ghashiyah

Sura Al-Ghashiyah (الغاشية) ni sura ya 88 ya Qur'ani. Ina aya 26 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, الغاشية, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-Ghashiyah

Sura Al-Ghashiyah ina aya ngapi?

Sura Al-Ghashiyah ina aya 26.

Je, Sura Al-Ghashiyah ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-Ghashiyah iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-Ghashiyah iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-Ghashiyah wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp