Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 87 ya Qur'ani

Sura Al-A'la

Makkiyya Aya 19 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَبِّحِ ٱسْمَ رَبِّكَ ٱلْأَعْلَى ﴿١﴾

Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,

ٱلَّذِى خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾

Aliye umba, na akaweka sawa,

وَٱلَّذِى قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾

Na ambaye amekadiria na akaongoa,

وَٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾

Na aliye otesha malisho,

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾

Kisha akayafanya makavu, meusi.

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ ﴿٦﴾

Tutakusomesha wala hutasahau,

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾

Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾

Na tutakusahilishia yawe mepesi.

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾

Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾

Atakumbuka mwenye kuogopa.

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلْأَشْقَى ﴿١١﴾

Na atajitenga mbali nayo mpotovu,

ٱلَّذِى يَصْلَى ٱلنَّارَ ٱلْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾

Ambaye atauingia Moto mkubwa.

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾

Tena humo hatakufa wala hawi hai.

قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾

Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.

وَذَكَرَ ٱسْمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾

Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.

بَلْ تُؤْثِرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا ﴿١٦﴾

Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!

وَٱلْءَاخِرَةُ خَيْرٌۭ وَأَبْقَىٰٓ ﴿١٧﴾

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

إِنَّ هَٰذَا لَفِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ ﴿١٨﴾

Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,

صُحُفِ إِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾

Vitabu vya Ibrahimu na Musa.

Al-A'la Aya 1 kati ya 19

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-A'la

Sura Al-A'la (الأعلى) ni sura ya 87 ya Qur'ani. Ina aya 19 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, الأعلى, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-A'la

Sura Al-A'la ina aya ngapi?

Sura Al-A'la ina aya 19.

Je, Sura Al-A'la ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-A'la iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-A'la iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-A'la wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp