وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ ﴿١﴾
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
Sura ya 86 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ ﴿١﴾
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ ﴿٢﴾
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
ٱلنَّجْمُ ٱلثَّاقِبُ ﴿٣﴾
Ni Nyota yenye mwanga mkali.
إِن كُلُّ نَفْسٍۢ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌۭ ﴿٤﴾
Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾
Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّآءٍۢ دَافِقٍۢ ﴿٦﴾
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
يَخْرُجُ مِنۢ بَيْنِ ٱلصُّلْبِ وَٱلتَّرَآئِبِ ﴿٧﴾
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجْعِهِۦ لَقَادِرٌۭ ﴿٨﴾
Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
يَوْمَ تُبْلَى ٱلسَّرَآئِرُ ﴿٩﴾
Siku zitakapo dhihirishwa siri.
فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٍۢ وَلَا نَاصِرٍۢ ﴿١٠﴾
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجْعِ ﴿١١﴾
Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
وَٱلْأَرْضِ ذَاتِ ٱلصَّدْعِ ﴿١٢﴾
Na kwa ardhi inayo pasuka!
إِنَّهُۥ لَقَوْلٌۭ فَصْلٌۭ ﴿١٣﴾
Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
وَمَا هُوَ بِٱلْهَزْلِ ﴿١٤﴾
Wala si mzaha.
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًۭا ﴿١٥﴾
Hakika wao wanapanga mpango.
وَأَكِيدُ كَيْدًۭا ﴿١٦﴾
Na Mimi napanga mpango.
فَمَهِّلِ ٱلْكَٰفِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًۢا ﴿١٧﴾
Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura At-Tariq (الطارق) ni sura ya 86 ya Qur'ani. Ina aya 17 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, الطارق, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura At-Tariq ina aya 17.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura At-Tariq iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.