وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾
Naapa kwa usiku unapo funika!
Sura ya 92 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾
Naapa kwa usiku unapo funika!
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾
Na mchana unapo dhihiri!
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ ﴿٣﴾
Na kwa Aliye umba dume na jike!
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَٱتَّقَىٰ ﴿٥﴾
Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
وَصَدَّقَ بِٱلْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾
Na akaliwafiki lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾
Tutamsahilishia yawe mepesi.
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
وَكَذَّبَ بِٱلْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾
Na akakanusha lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾
Tutamsahilishia yawe mazito!
وَمَا يُغْنِى عَنْهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ ﴿١١﴾
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ ﴿١٢﴾
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
وَإِنَّ لَنَا لَلْءَاخِرَةَ وَٱلْأُولَىٰ ﴿١٣﴾
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًۭا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
لَا يَصْلَىٰهَآ إِلَّا ٱلْأَشْقَى ﴿١٥﴾
Hatauingia ila mwovu kabisa!
ٱلَّذِى كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾
Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلْأَتْقَى ﴿١٧﴾
Na mchamngu ataepushwa nao,
ٱلَّذِى يُؤْتِى مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعْمَةٍۢ تُجْزَىٰٓ ﴿١٩﴾
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِ ٱلْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾
Naye atakuja ridhika!
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Al-Layl (الليل) ni sura ya 92 ya Qur'ani. Ina aya 21 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, الليل, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Al-Layl ina aya 21.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Al-Layl iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.