وَٱلضُّحَىٰ ﴿١﴾
Naapa kwa mchana!
Sura ya 93 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلضُّحَىٰ ﴿١﴾
Naapa kwa mchana!
وَٱلَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾
Na kwa usiku unapo tanda!
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
وَلَلْءَاخِرَةُ خَيْرٌۭ لَّكَ مِنَ ٱلْأُولَىٰ ﴿٤﴾
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰٓ ﴿٥﴾
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًۭا فَـَٔاوَىٰ ﴿٦﴾
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
وَوَجَدَكَ ضَآلًّۭا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾
Na akakukuta umepotea akakuongoa?
وَوَجَدَكَ عَآئِلًۭا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
فَأَمَّا ٱلْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾
Basi yatima usimwonee!
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Ad-Duha (الضحى) ni sura ya 93 ya Qur'ani. Ina aya 11 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, الضحى, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Ad-Duha ina aya 11.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Ad-Duha iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.