أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾
Hatukukunjulia kifua chako?
Sura ya 94 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾
Hatukukunjulia kifua chako?
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾
Na tukakuondolea mzigo wako,
ٱلَّذِىٓ أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾
Ulio vunja mgongo wako?
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾
Na tukakunyanyulia utajo wako?
فَإِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾
Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
إِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًۭا ﴿٦﴾
Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
فَإِذَا فَرَغْتَ فَٱنصَبْ ﴿٧﴾
Na ukipata faragha, fanya juhudi.
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرْغَب ﴿٨﴾
Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Ash-Sharh (الشرح) ni sura ya 94 ya Qur'ani. Ina aya 8 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, الشرح, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Ash-Sharh ina aya 8.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Ash-Sharh iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.