Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 84 ya Qur'ani

Sura Al-Inshiqaq

Makkiyya Aya 25 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتْ ﴿١﴾

Itapo chanika mbingu,

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,

وَإِذَا ٱلْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾

Na ardhi itakapo tanuliwa,

وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾

Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,

يَٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًۭا فَمُلَٰقِيهِ ﴿٦﴾

Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.

فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ ﴿٧﴾

Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًۭا يَسِيرًۭا ﴿٨﴾

Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًۭا ﴿٩﴾

Na arudi kwa ahali zake na furaha.

وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهْرِهِۦ ﴿١٠﴾

Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,

فَسَوْفَ يَدْعُوا۟ ثُبُورًۭا ﴿١١﴾

Basi huyo ataomba kuteketea.

وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾

Na ataingia Motoni.

إِنَّهُۥ كَانَ فِىٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾

Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.

إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾

Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.

بَلَىٰٓ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًۭا ﴿١٥﴾

Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!

فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلشَّفَقِ ﴿١٦﴾

Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,

وَٱلَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾

Na kwa usiku na unavyo vikusanya,

وَٱلْقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ ﴿١٨﴾

Na kwa mwezi unapo pevuka,

لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍۢ ﴿١٩﴾

Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!

فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾

Basi wana nini hawaamini?

84:21 Aya ya sajda

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ ٱلْقُرْءَانُ لَا يَسْجُدُونَ ۩ ﴿٢١﴾

Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾

Bali walio kufuru wanakanusha tu.

وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾

Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.

فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾

Basi wabashirie adhabu chungu!

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍۭ ﴿٢٥﴾

Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.

Al-Inshiqaq Aya 1 kati ya 25

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-Inshiqaq

Sura Al-Inshiqaq (الانشقاق) ni sura ya 84 ya Qur'ani. Ina aya 25 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, الانشقاق, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-Inshiqaq

Sura Al-Inshiqaq ina aya ngapi?

Sura Al-Inshiqaq ina aya 25.

Je, Sura Al-Inshiqaq ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-Inshiqaq iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-Inshiqaq iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-Inshiqaq wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp