إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ ﴿١﴾
Mbingu itapo chanika,
Sura ya 82 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ ﴿١﴾
Mbingu itapo chanika,
وَإِذَا ٱلْكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتْ ﴿٢﴾
Na nyota zitapo tawanyika,
وَإِذَا ٱلْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾
Na bahari zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا ٱلْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
Na makaburi yatapo fukuliwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌۭ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
يَٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ ﴿٦﴾
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
فِىٓ أَىِّ صُورَةٍۢ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ ﴿٩﴾
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَٰفِظِينَ ﴿١٠﴾
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
كِرَامًۭا كَٰتِبِينَ ﴿١١﴾
Waandishi wenye hishima,
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾
Wanayajua mnayo yatenda.
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍۢ ﴿١٣﴾
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
وَإِنَّ ٱلْفُجَّارَ لَفِى جَحِيمٍۢ ﴿١٤﴾
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ ٱلدِّينِ ﴿١٥﴾
Wataingia humo Siku ya Malipo.
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَآئِبِينَ ﴿١٦﴾
Na hawatoacha kuwamo humo.
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ ﴿١٧﴾
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ ﴿١٨﴾
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌۭ لِّنَفْسٍۢ شَيْـًۭٔا ۖ وَٱلْأَمْرُ يَوْمَئِذٍۢ لِّلَّهِ ﴿١٩﴾
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Al-Infitar (الانفطار) ni sura ya 82 ya Qur'ani. Ina aya 19 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, الانفطار, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Al-Infitar ina aya 19.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Al-Infitar iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.