ٱقْرَأْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ ﴿١﴾
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
Sura ya 96 ya Qur'ani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱقْرَأْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ ﴿١﴾
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
خَلَقَ ٱلْإِنسَٰنَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
ٱقْرَأْ وَرَبُّكَ ٱلْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلْقَلَمِ ﴿٤﴾
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
عَلَّمَ ٱلْإِنسَٰنَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
كَلَّآ إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ لَيَطْغَىٰٓ ﴿٦﴾
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
أَن رَّءَاهُ ٱسْتَغْنَىٰٓ ﴿٧﴾
Akijiona katajirika.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجْعَىٰٓ ﴿٨﴾
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
Umemwona yule anaye mkataza
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰٓ ﴿١٠﴾
Mja anapo sali?
أَرَءَيْتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلْهُدَىٰٓ ﴿١١﴾
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
أَوْ أَمَرَ بِٱلتَّقْوَىٰٓ ﴿١٢﴾
Au anaamrisha uchamngu?
أَرَءَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ ﴿١٣﴾
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًۢا بِٱلنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
نَاصِيَةٍۢ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍۢ ﴿١٦﴾
Shungi la uwongo, lenye makosa!
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُۥ ﴿١٧﴾
Basi na awaite wenzake!
سَنَدْعُ ٱلزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
Nasi tutawaita Mazabania!
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَٱسْجُدْ وَٱقْتَرِب ۩ ﴿١٩﴾
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!
Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.
Sura Al-'Alaq (العلق) ni sura ya 96 ya Qur'ani. Ina aya 19 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.
Jina lake, العلق, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.
Sura Al-'Alaq ina aya 19.
Uainishaji: Makkiyya.
Sura Al-'Alaq iko katika Juzuu 30.
Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.