Muslim Flow iko kwenye majaribio na inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Pakua

Sura ya 80 ya Qur'ani

Sura 'Abasa

Makkiyya Aya 42 Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ ﴿١﴾

Alikunja kipaji na akageuka,

أَن جَآءَهُ ٱلْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

Kwa sababu alimjia kipofu!

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ ﴿٣﴾

Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكْرَىٰٓ ﴿٤﴾

Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?

أَمَّا مَنِ ٱسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾

Ama ajionaye hana haja,

فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾

Wewe ndio unamshughulikia?

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾

Na si juu yako kama hakutakasika.

وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾

Ama anaye kujia kwa juhudi,

وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾

Naye anaogopa,

فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾

Ndio wewe unampuuza?

كَلَّآ إِنَّهَا تَذْكِرَةٌۭ ﴿١١﴾

Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ ﴿١٢﴾

Basi anaye penda akumbuke.

فِى صُحُفٍۢ مُّكَرَّمَةٍۢ ﴿١٣﴾

Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,

مَّرْفُوعَةٍۢ مُّطَهَّرَةٍۭ ﴿١٤﴾

Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.

بِأَيْدِى سَفَرَةٍۢ ﴿١٥﴾

Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,

كِرَامٍۭ بَرَرَةٍۢ ﴿١٦﴾

Watukufu, wema.

قُتِلَ ٱلْإِنسَٰنُ مَآ أَكْفَرَهُۥ ﴿١٧﴾

Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?

مِنْ أَىِّ شَىْءٍ خَلَقَهُۥ ﴿١٨﴾

Kwa kitu gani amemuumba?

مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ ﴿١٩﴾

Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.

ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ ﴿٢٠﴾

Kisha akamsahilishia njia.

ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقْبَرَهُۥ ﴿٢١﴾

Kisha akamfisha, akamtia kaburini.

ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ ﴿٢٢﴾

Kisha apendapo atamfufua.

كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَآ أَمَرَهُۥ ﴿٢٣﴾

La! Hajamaliza aliyo muamuru.

فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ ﴿٢٤﴾

Hebu mtu na atazame chakula chake.

أَنَّا صَبَبْنَا ٱلْمَآءَ صَبًّۭا ﴿٢٥﴾

Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,

ثُمَّ شَقَقْنَا ٱلْأَرْضَ شَقًّۭا ﴿٢٦﴾

Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,

فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا حَبًّۭا ﴿٢٧﴾

Kisha tukaotesha humo nafaka,

وَعِنَبًۭا وَقَضْبًۭا ﴿٢٨﴾

Na zabibu, na mimea ya majani,

وَزَيْتُونًۭا وَنَخْلًۭا ﴿٢٩﴾

Na mizaituni, na mitende,

وَحَدَآئِقَ غُلْبًۭا ﴿٣٠﴾

Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,

وَفَٰكِهَةًۭ وَأَبًّۭا ﴿٣١﴾

Na matunda, na malisho ya wanyama;

مَّتَٰعًۭا لَّكُمْ وَلِأَنْعَٰمِكُمْ ﴿٣٢﴾

Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ ﴿٣٣﴾

Basi utakapo kuja ukelele,

يَوْمَ يَفِرُّ ٱلْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾

Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,

وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾

Na mamaye na babaye,

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾

Na mkewe na wanawe -

لِكُلِّ ٱمْرِئٍۢ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍۢ شَأْنٌۭ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.

وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۢ مُّسْفِرَةٌۭ ﴿٣٨﴾

Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,

ضَاحِكَةٌۭ مُّسْتَبْشِرَةٌۭ ﴿٣٩﴾

Zitacheka, zitachangamka;

وَوُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌۭ ﴿٤٠﴾

Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾

Giza totoro litazifunika,

أُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَفَرَةُ ٱلْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾

Hao ndio makafiri watenda maovu.

'Abasa Aya 1 kati ya 42

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura 'Abasa

Sura 'Abasa (عبس) ni sura ya 80 ya Qur'ani. Ina aya 42 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, عبس, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura 'Abasa

Sura 'Abasa ina aya ngapi?

Sura 'Abasa ina aya 42.

Je, Sura 'Abasa ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura 'Abasa iko katika Juzuu ipi?

Sura 'Abasa iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura 'Abasa wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Abdur-Rahman As-Sudais, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

WhatsApp